MWONGOZO WA TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

MWONGOZO WA TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

TUMBO LISILOSHIBA —Said A. Mohamed


Hadithi inaanza kwa taharuki kuhusu uvumi uliogeuka mnong'ono ukaeneza wasiwasi-hofu. Wasiwasi ulikuwa vibanda vitabomolewa vote. Watu wakubwa walitaka kuchukua makao ya watu ili kuendeleza ujenzi wao. Kwa Mzee Mago ndiko kituo cha kuzungumzia juu ya haki zao. Yeye huwakusanya wenzake iii wajadili juu ya haki zao za kuishi pale wanapochagua.
Wanahojiana mambo juu ya:
Kustahili kuishi kwa amani na furaha popote nchini mwao.
Namna ya kuruka vikwazo vya sheria vilivyowekwa ili watu wadogo wasiweze kupoteza mali zao.
Kushawishiana watafute wanasheria waaminifu iii kutatua (mazonge ya sheria). Wanadai kuwa wanasheria waaminifu wameadimika —hakuna haki siku hizi.
Kunasihiana na kuamshana juu ya kukubali maendeleo yanayopiga kasi nchini mwao.
Maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu —mdogo kwa mkubwa, wa kike kwa wa kiume.
Mtu hawezi kukimbia ukweli, upya na usasa hutazamiwa kuleta mafanikio kwa watu wote. Mzee Mago huwaonya wauchunguze huo upya na usasa waujue jmst uhvyokaa —utaleta faida au hasara. Umaskini sio ujinga. Watu maskini wangeshauriwa wangeweza kuonyesha watakavyochangia maendeleo ya nchi yao. Watu wadogo hukasirika kwani wao hufanywa kuwa kama takataka. Hasira yao ndiyo inayowapa motisha wa kusema na kujitetea. Wakubwa walidai
kuwa jiji limejaa na halina nafasi tens, suluhisho ni kubomoa baadhi ya mitaa. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, majumba ya Mall, maduka n k. Kwa hiyo, suluhisho la uhaba wa nafasi jijini ni kubomoa sehemu zingine. Mzee Mago aliwaleta wenzake pamoja kupigania haki za hapo Madongoporomoka —pasibomolewe.
Baadhi ya wanyonge hawa wanataka wapewe visenti vyao vichache vaondoke. Wengine wanadai, hakuna kuondoka. Wanataka vvabaki pale pale na kupigania haki zao. Kabwe alisisitiza kwa nguvu kuwa wakubwa hawataweza, kwani wanaogopa umma wa Madongoporomoka. Bi. Suruta aliwatahadharisha kuwa wakubwa hawaogopi kitu chochote.
Wakati mjadala ukiendelea, chakula cha pale mgahawani kilikuwa tayari na kikaanza kunukia na kuwatamanisha wale waliobarizi hapo. Mara likatokea jitu kubwa na kukaa mle ndani. Jitu hilo liliamuru liletewe chakula Chote cha wateja wa Mzee Mugo. Jitu hilo lilifagia aina zote za vyakula: wali wa nazi, mchuzi, nyama ya kuchoma, kachumbari n k.
Baada ya kula vyakula vyote vya mgahawani hapo lililipa hela yote kisha likaahidi kuwa kesho tena lingekuja na liandaliwe chakula mara mbili ya kile kilicholiwa. Likawaacha kwa kitendawili kuwa, kesho kama wakiamka salama kama watafungua milango ya nyumba zao zilizosimama juu ya ardhi adhimu.
Alfajiri iliyofuata, polisi wakiwa na mirau na bunduki walikuwa wanalinda askari wa baraza la mji wakiviporomosha vibanda vyote.
Kulikuwa na mahangaiko ya wanyonge wasiwasi na hatan Mbio... Hawajui waokoe mali zao duni au nafsi zao kelele' kwenzi vilio, malalamiko, vumbi (Uk 10).
Kumbe kile kitendawili cha jitu kilimaanisha kuwa ardhi Yao ingetwaliwa yote. Hata hivyo, wanyone wanashikilia msimamO wao kuwa fujo zisingeweza kuwaondoa katikia ardhi yao.
Baada ya wiki tatu za vurugu hilo; vibanda mshenzi Vya MadongoporomOka viliota, tena vingi kuliko vya awali.

Comments

Popular Posts